KUZUIA BARUA ZA UHAMISHO NI UHALIFU – MKOMI
TMC NEWS TV
0:00 / 0:00
KUZUIA BARUA ZA UHAMISHO NI UHALIFU – MKOMI
1 173 просмотра · 4 месяца назад
TMC NEWS TV
42,3 тыс. подписчиков
1 173 просмотра · 4 месяца назад
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Juma Mkomi, amewataka Wakuu wa Taasisi na Wakurugenzi kuacha kuzuia barua za uhamisho wa watumishi wa umma, akieleza kuwa kufanya hivyo ni kosa linalokiuka taratibu za utumishi wa umma.
Bw. Mkomi amesema Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ndiyo yenye mamlaka ya kuhamisha watumishi wa umma, hivyo kiongozi yeyote anayezuia barua hizo anawanyima watumishi haki yao ya msingi kwa mujibu wa sheria na kanuni za utumishi wa umma.
#UtumishiWaUmma #UhamishoWaWatumishi #SerikaliYaTanzania #UtawalaBora #ofisiyarais