Перейти к содержимому

96 MBARONI YUMO SAMWELI NA ABDALLAH "KILLER"

ZANZIBAR YETU

0:00 / 0:00

96 MBARONI YUMO SAMWELI NA ABDALLAH "KILLER"

2 184 просмотра · 1 дн. назад
ZANZIBAR YETU
10,8 тыс. подписчиков
2 184 просмотра · 1 дн. назад
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi lilifanya operesheni mbalimbali na kufanikiwa kuwakamata jumla ya watuhumiwa 96 kwa tuhuma za makosa mbalimbali ya jinai. Miongoni mwao wapo watuhumiwa wa mauaji, unyang’anyi, ubakaji, wizi wa pikipiki, dawa za kulevya na kupatikana na pombe za kienyeji (gongo). Miongoni watuhumiwa waliokamatwa ni:- Mtuhumiwa wa mauaji aitwaye Samweli John Raphael (28) mkazi wa Dar es salaam ambaye mwezi Septemba 2025 alimshambulia Mohamed George Gasper (22) mkazi wa Shakani, Wilaya ya Magharibi B” aliyekuwa dereva wa pikipiki kwa kumpiga na kitu butu sehemu ya kichwani na kumsababishia jeraha kubwa lililopelekea kufariki dunia. Mtuhumiwa baada ya kutekeleza tukio hilo alikimbia nje ya Zanzibar na baada ya ufuatiliaji Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi kwa kushirikiana na Polisi Mkoa wa Pwani mtuhumiwa alikamatwa akiwa mafichoni Wilaya ya kisarawe Mkoa Pwani.