MALARIA YAONGEZEKA MIGOMBANI, WATAALAMU WA AFYA WAINGIA KAZINI
ASAM Online TV
0:00 / 0:00
MALARIA YAONGEZEKA MIGOMBANI, WATAALAMU WA AFYA WAINGIA KAZINI
403 просмотра · 4 дн. назад
ASAM Online TV
22,4 тыс. подписчиков
403 просмотра · 4 дн. назад
Malaria ni miongoni mwa magonjwa yanayoendelea kupewa kipaumbele katika juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar za kudhibiti na hatimaye kutokomeza ugonjwa huo.
Katika hatua hiyo, Timu ya Afya Wilaya ya Mjini kwa kushirikiana na Kitengo cha Kutokomeza Malaria imeendesha zoezi la kupuliza dawa katika Shehia ya Migombani, eneo la Msikiti Ruba, kufuatia kuongezeka kwa kesi za Malaria katika eneo hilo.
Akizungumza baada ya zoezi hilo, Afisa Afya Wilaya ya Mjini, Nasra Mohammed Makame, amesema hatua hiyo inalenga kuzuia kuendelea kuongezeka kwa maambukizi ya Malaria, kutokana na kuwepo kwa mazingira yanayochochea mazalia ya mbu katika eneo hilo.
Amesema wananchi wanapaswa kushirikiana na wataalamu wa afya katika kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na salama, pamoja na kuchukua hatua za kujikinga dhidi ya Malaria.
#AsamOnlineTV #ZanzibarNews #Malaria #KutokomezaMalaria #Afya #Migombani #AfyaZanzibar #Zanzibar #HabariZanzibar #NewsUpdate #Trending