Перейти к содержимому

UKUTA WA MITA 500 KUJENGWA UROA KUNUSURU MAKAAZI YA WANANCHI

ZANZIBAR YETU

0:00 / 0:00

UKUTA WA MITA 500 KUJENGWA UROA KUNUSURU MAKAAZI YA WANANCHI

2 867 просмотров · 1 дн. назад
ZANZIBAR YETU
10,8 тыс. подписчиков
2 867 просмотров · 1 дн. назад
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, amesema kwamba Zanzibar imekabiliwa na tatizo kubwa la athari za mabadiliko ya tabia nchi ambapo serikali inafanya juhudi za kuchukua hatua stahiki juu ya namna ya kulikabili ili kutondosha athari kwa jamii zizotokana na hali hiyo. Othman ameyasema hayo kwa nyakati tofauti kwenye muendelezo wa zaiara katika taasisi zilizochini ya ofisi yake alipotembelea katika Vijiji vya Chwaka na Uroa wilaya ya Kati Unguja kuona maji ya bahari yanavyoingia kwenye makaazi ya wananchi na kuathiri shughuli za kijamii. Amesema kwamba suala hilo limekuwa likichangiwa na shughuli za kijamii ikiwemo ukulima ,ujenzi holela na ukataji wa mikoko na kuharibiwa kwa matumbawe huku dunia nayo ikichangia kuongezeka kwa hali ya joto duniani na kusababisha kuyayuka kwa theluji jambo linaloleta athari kubwa hasa kwa nchi kama Zanzibar. Amefahamisha kwamba hali hiyo imekuwa ikisababisha bahari pia kuchafuka na baadhi ya viumbe muhimu wa baharini kutoweka kutokana na kuongezeka kwa joto la bahari kunakotokana na matendo hayo ya wananchi na shughuli za kidunia. Othman amesema nchi za visiwa kama vile Zanzibar , Maldive , nchi ya Uholanzi na kwengineko duniani ni miongoni mwa nchi zinzoshuhudia athari kubwa itokanayo na mabadiliko ya tabia nchi na kwamba serikali kwa kushirikiana na wadau mbali mbali imekuwa ikifanya juhudi kulikabilia tatizo hilo. Hata hivyo, amewahidi wakaazi wa kijiji cha Uroa kwamba serikali itahakikisha kwamba inafanya juhudi za kuzuia athari za tatizo hilo katika kijiji hicho kwa kujengwa ukuta utakaopunguza maji ya bahari kuingia kwenye makazi ya wananchi. Amesema kwamba serikali itataoa fedha katika kuhakikisha kwamba suala hilo la ujenzi wa ukuta uroa linatekelezwa ipasavyo pamoja na kuzingatia kuutumia mpango makhusi wa serikali kukabili changamoto za aina hiyo katika maeneo yote 148 ya Unguja na Pemba. Amewataka wananchi kujitahidi kushirikiana na serikali katika kuhakikisha kwamba juhudi za pamoja zinafanyika kulikabili tatizo hilo ikiwa ni pamoja na kuzia kutendeka shughuli za kijamii zinazochangia kasi ya mabadiliko ya tabia nchi. Aidha Mhe. Othman amesema kwamba serikali inafikiria kutumia mpango wa ufukiaji wa bahari ili kupata ardhi kubwa Zaidi inayoweza kutumika kwa shughuli za kijamii kama inavyofanyika katika nchi mbali mbali duniani kwa kuwa ni jambo linalowezekana kitaalamu. Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Ana Athanas Poul amesema kwamba serikali kupitia Ofisi hiyo inaendelea kupita katika maeneo mbali mbali na kwamba juhudi zinaelekezwa katika kunusuru makazi ya wananchi yasiathiriwe na mabadiliko ya tabia nchi. Amesema kwamba wananchi wanapaswa kushirikiana na serikali katika kuhakikisha wanapanda miti na kuitunza ikiwemo ya mikoko na kuzuia uharibuvu wa matumbawe jambo litakalosaidia sana kupunguza athari za tatizo hilo. Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mazingira Farhat Mbarouk amesema kwamba eneo hilo la uroa limekuwa likifikwa na maji mara mbili kila mwaka na kwamba kwa ufadhili wa Benki ya Dunia kutajengwa ukuta wenye urefu wa mita 500 katika utekelezaji wa awamu mbili tofauti. Amesema kwamba hatua hiyo itasaidia kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi katika eneo hilo na kusaidia kupunguza uharibifu wa makaazi ya wananchi wa kijiji hicho cha uroa. Wakati huo huo Mhe. Othman alitembelea Skuli Mjumuishi huko Jendele wilaya ya kati Unguja na ameushauri uongozi wa Wizara ya elimu kufanya matayarisho ya kuwasaidia wawekezaji wa sekta ya elimu watakayojitokeza kuanzisha skuli mjumuishi za binafasi na kwa watoto wenye mahitaji maalum. Amesema kwamba juhudi kubwa za serikali zilizoanzishwa kusomesha watoto wenye mahitaji maalumu itasaidia miaka michache ijayo kuwepo wataalamu wengi wataokuwa na uwezo wa kuingia katika sekta mbali mbali zikiwemo za binafasi. Naye katibu Mkuu wa wizara ya Elimu Zanzibar Khaimis Abdalla said amsesma kwamba upo uwezekano wa kuwafunza vijana kupitia elimu mjumuishi na kupata fursa kubwa katika siku zijazo kuweza kupatikana wataalamu wa fani mbali mbali kutoka kwenye kundi la watu wa jamii hiyo. Othman katika ziara hiyo ametembelea Kijiji cha uroa na chwaka kuoana athari za mabadiliko ya tabia nchi, pia kuona namna ya utoaji wa elimu mjumuishi katika skuli ya aina hiyo iliyopo Jendele na kumalizia ziara yake katika eneo linalokusudiwa kujengwa kituo kikubwa cha Watu wenye mahitaji maalim kinachosimamiwa na baraza la watu wenye Ulemavu huko Kibele wilaya ya Kati Unguja.